Simba vs Vipers
Habari za michezo

LIGI YA MABINGWA AFRIKA…SIMBA NDIO KWANZAA KUNAKUCHA…HOROYA AKIONA CHA MTEMA KUNI…

admin March 8, 2023 9:27 am

BAO la Clatous Chama alilofunga dakika ya 45 limetosha kuipa Simba ushindi katika mchezo wao dhidi ya Vipers uliochezwa jana katika uwanja wa Mkapa.

Chama alifunga bao hilo akitumia vizuri pasi ya Moses Phiri ambaye alimpenyezea na yeye kuweka wavuni.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi sita na mabao mawili ikishika nafasi ya pili katika kundi C huku nafasi ya kwanza ikiwa ni Raja Casablanca ikiwa na pointi 12 baada ya kuichapa Horoya mabao 3-1 jana.

Simba imeendeleza ubabe kwa Vipers kwenye mechi mbili mfululizo ikishinda nyumbani na ugenini katika hatua hii ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mchezo wa kwanza nchini Uganda, Simba ilishinda 1-0 bao likifungwa na Henoc Inonga na kwenye mchezo wa Mkapa imeshinda tena 1-0.

Nafasi ya tatu ipo Horoya ikiwa na pointi nne huku Vipers ikishika mkia ikiwa na pointi moja pekee.

Simba itakuwa barua kingine cha kusaka pointi tatu mbele ya Horoya Machi 18 katika uwanja wa Mkapa huku Vipers ikiisubiri Raja Casablanca nchini Uganda.

KUHUSU MECHI NA WAMALI KESHO….NABI KUIBUKA NA MBINU HIZI ZA KIJASUSI KWA MKAPA… KOCHA WA CHELSEA AFUNGA SAFARI MPAKA BONGO KUMTAZAMA MUSONDA LEO…ALIANZA NA CHAMA JANA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply