Home Habari za michezo PETER BANDA AZIDI KUIPAISHA SIMBA KIMATAIFA… ATAJWA KAMA MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI AFRIKA…

PETER BANDA AZIDI KUIPAISHA SIMBA KIMATAIFA… ATAJWA KAMA MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI AFRIKA…


Nyota wa Simba, Peter Banda amechaguliwa na Shirikisho la Soka Afrika ngazi ya mashindano ya klabu kwa maana ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika kama kinda bora akiyefanya vizuri kwenye michuano hiyo msimu uliopita 2021/2022.

Banda mwenye umri wa miaka 21 ametajwa sambamba na makinda wengine watatu Mkongomani Guy Mbenza (22) anayecheza kwa mkopo Wydad Casablanca kwa mkopo akitokea Royal Antwerp ya Ubelgiji aliyokuwa akiichezea Mtanzania Mbwana Samatta msimu uliopita.

Wengine ni Mmisri Ahmed AbdelKader (23) anayecheza Al Ahly Mmorocco, Mouad Fekkak anayekipiga RS Berkane ya nchini kwao huko.

Banda alisajiliwa na Simba mwanzoni mwa msimu uliomalizika akitokea Sheriff Tiraspol alikokuwa kwa mkopo akitokea Big Bullets ya nchini kwao Malawi ambayo ndio ilimuuza kwa Wekundu wa Msimbazi hao.

Huenda Banda msimu ujao akafanya makubwa zaidi katika michuano hiyo baada ya Simba kumaliza ligi katika nafasi ya pili na kujihakikishia kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo itaanzia hatua ya mwanzo.

SOMA NA HII  TYR AGAIN:- KAMA AL AHLY WALIPATA BAHATI DAR....NA SISI TUNAWEZA KUPATA BAHATI MISRI...