Habari za michezo

UCHAGUZI MKUU YANGA: DK MSOLA AWAPA ‘ZA USO’ WANACHAMA UKUMBINI…..ATAJA SABABU ZA KUJIWEKA KANDO ….

admin July 9, 2022 12:43 pm


MWENYEKITI anayemaliza muda wake Mshindo Msola amewataka wajumbe kufanya maamuzi sahihi katika uchaguzi wa viongozi wao watakaoiongoza vyema timu yao.

Msola ameyasema hayo leo wakati akitoa neno kwa Wanayanga katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere unapofanyika uchaguzi.

Msola amesema anaamini kura zikienda kwa watu sahihi itasaidia kuendeleza pale ambapo yeye na wajumbe wanaomaliza muda wao walipiishia.

“Sitegemei kugombea nafasi yoyote, nitabakia kuwa mwanayanga mwaminifu nitaendelea kuwa mwanachama mwaminifu,” anasema Msola.

Aidha Msola amewatakia kila la heri waliokuwa wajumbe wenzake ambao wamejitosa kuwania nafasi hizo kwa mara nyingine akiamini wanaweza kutokana na kazi kubwa walioifanya.

“Leo ni siku muhimu sana katika maisha yangu maana katika kampeni zangu nilitaka suala la mabadiliko ya kiuendeshaji na leo ndio uchaguzi unaenda kuwaweka viongozi hao madarakani ni jambo la kujivunia sana sana”. amesema Msola.

FAMILIA WAANIKA KILICHOMUUA BI HINDU….ALIKUWA AKIPUMULIA MASHINE NYUMBANI…”ALIKUWA NA WATU WENGI”… UCHAGUZI MKUU YANGA: MANARA ATANGAZA ‘SAPRAIZI’ KUBWA KWA MASHABIKI….UKUMBI MZIMA WALIPUKA KWA SHANGWE….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply