Habar za Usajili Simba

ACHANA NA OKRAH….BADO MAJEMBE HAYA MAWILI YANASUBIRI KUTAMBULISHWA SIMBA….NCHI ITASIMAMA….

admin July 13, 2022 12:51 pm


KLABU ya Simba imenasa saini ya kiungo mshambuliaji, Augustine Okrah kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Bechem United ya Ghana.

Nyota huyo aliyeonyesha kiwango kizuri msimu ulioisha akiwa na timu hiyo unakuwa ni usajili wa tatu kwa wachezaji wa kigeni baada ya kuwatambulisha Moses Phiri kutoka Zanaco ya Zambia na Victor Akpan aliyekuwa anaichezea timu ya Coastal Union.

Mbali na usajili huo kwa wageni ila wapo wazawa wawili waliotambulishwa na kikosi hicho chini ya kocha wake, Zoran Maki ambao ni Mshambuliaji, Habib Kyombo aliyetoka Mbeya Kwanza na nyota mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani Nassoro Kapama kutoka Kagera Sugar.

Katika Ligi ya Ghana Okrah amehusika kwenye mabao 17 akiwa na Bechem ambapo amefunga 14 na kutoa pasi (Assisti) tatu katika michezo 31 aliyocheza huku akitarajiwa kuungana na kikosi hicho kinachoelekea Misri kesho kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Tunafahamu kwamba nyota wengine ambao wamejiunga na miamba hiyo ni mshambuliaji raia wa Afrika ya Kati  Cesar Manzoki kutoka (Vipers FC) na Nelson Okwa wa Rivers United.

KISA MSUVA KULIPWA BILION 1.6….FAMILIA YAKE NZIMA WAANGUKA NA KULIA…BABAKE AFUNGUKA WALIVYOMPIGANIA… BAADA YA KUHAKIKISHIWA KUPATA BILION 1.6 KUTOKA KWA WAARABU….MSUVA AANZA KUZIPANGIA MATUMIZI ‘CHAP HARAKA’…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply