Habari za michezo

KOCHA MPYA SIMBA AZUA KIZAAZAA…AKATAA KUKUBALI MALENGO YA KLABU YA KUFIKA NUSU FAINAL CAF…

admin July 13, 2022 5:20 pm


MSEMAJI wa klabu ya Simba, Ahmed Ally ameweka wazi timu yao kwenda kuweka kambi nchini Misri katika mji wa Ismailia kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Hoteli ya Serena, Ahmed amesema safari ya kwenda Misri itaanza rasmi tarehe 14 Julai.

“Tunaondoa tarehe 14 mwezi huu na tutakuwa na tarehe tano mwezi wa nane tutarudi kwa ajili ya Simba Day pamoja na mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa Ligi,” amesema Ahmed na kuongeza;

“Tutakuwa na wachezaji wote kasoro wale ambao watakuwa kwenye timu za Taifa ambao tutawaacha wakiwa na majukumu mengine.”

Akizungumzia upande wa kocha wao mpya amesema wamempa mkataba wa mwaka mmoja na anatakiwa kuhakikisha Simba inapata ubingwa wa Ligi Kuu.

“Zoran yupo hapa kuhakikisha Simba inapata ubingwa wa Ligi, Ngao ya Jamii na Kombe la Shirikisho pamoja na kuingia nusu fainali Caf,” amesema Ahmed.

Upande wa kocha mpya wa Simba, Zoran Manojnlovic ni kama amepinga kauli hiyo baada ya kusema upande wake hataki kuahidi makubwa.

Zoran amesema jambo kubwa la kwanza ni kuhakikisha timu hiyo inafika hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Sitaki kusema nitachukua ubingwa wa Afrika, mimi ahadi yangu ni kuhakikisha timu inafika hatua ya makundi halafu hatua zingine zinafuata.”

Zoran amesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mwingine kulingana na mwenendo wa timu.

BAADA YA MASHABIKI KUUPONDA USAJILI WAKE….IVO MAPUNDA AIBUKA NA UJUMBE HUU KWA KYOMBO…AMTAJA GEORGE MPOLE… BAADA YA KUMALIZANA NA SINGIDA BIG STARS..METACHA MNATA AIBUKA NA KUANIKA HAYA YASIYOFAHAMIKA NA WENGI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply