Habari za michezo

BAADA YA KUMALIZANA NA SINGIDA BIG STARS..METACHA MNATA AIBUKA NA KUANIKA HAYA YASIYOFAHAMIKA NA WENGI…

admin July 13, 2022 5:25 pm


BAADA ya kipa, Metacha Mnata kutambulishwa Singida Big Stars, amesema anachokizingatia ni kazi tu, ndio maana huduma yake inaonekana muhimu kwa timu zinazomtaka.

Hivi karibuni kupitia mtandao wa kijamii (Instagram) ya Singida Big Stars, miongoni mwa wachezaji waliyowatambulisha ni Metacha ambaye amesema mashabiki wasubiri kuona mchango wake.

“Ninapotoka timu moja kwenda nyingine ifahamike ni kazi ndiyo inafanya nionekane sehemu mbalimbali, nashukuru Mungu Polisi Tanzania nimefanya nao kazi vizuri msimu uliyoisha, hivyo maisha mengine yataendelea,” amesema Metacha na kuongeza;

“Ninachokizingatia kwenye karia yangu ni nidhamu, kujituma na kujitambua, naamini hivyo vinanisaidia kulinda kiwango changu.”

Mbali na hilo, amesema msimu uliyoisha umempa taswira ya nini afanye kufanya maandalizi ya msimu ujao, kuhakikisha huduma yake inakuwa muhimu kwenye timu.

“Mapumziko yangu muda mwingi nitautumia na familia yangu na nitakuwa nafanya mazoezi mepesi, baada ya hapo nitasubiri ratiba ya kuingia kambini,” amesema.

KOCHA MPYA SIMBA AZUA KIZAAZAA…AKATAA KUKUBALI MALENGO YA KLABU YA KUFIKA NUSU FAINAL CAF… UKWELI MCHUNGU….YANGA YA GSM NA YANGA YA MANJI UTOFAUTI WAKE NI HUU…SIMBA KIMFUMO BADO SANA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply