Habar za Usajili Simba

ZA NDAANI KABISAAA….ISHU YA KICHUYA KURUDI SIMBA …KILICHOBAKI NI KAMA KUMSUKUMA MLEVI…HAKIKISHA UNABANDO TU…

admin July 13, 2022 1:18 pm


HUENDA nyota wa zamani wa Simba, anayekipiga kwa sasa Namungo, Shiza Kichuya akarejea ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao kama kila kitu kitaenda sawa.

Taarifa zilizopo ni kuwa tayari winga huyo aliyetisha msimu huu na Wauaji wa Kusini hao akifunga jumla ya mabao manane kwenye ligi yupo jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo na baadhi ya mabosi wa Simba wanaotaka arudi.

Inaelezwa Kichuya na upande mmoja wa viongozi wa Simba wamekubaliana kila kitu hadi mshahara atakaoupata lakini kuna upande mwingine bado una wasiwasi na ubora wake kwani amewahi kuichezea timu hiyo kwa vipindi viwili tofauti.

“Ni suala la muda tu, anaweza kusaini wakati wowote shida iliyopo ni kwenye uongozi kuna baadhi ya watu wachache wana wasiwasi naye lakini kuhusu mambo ya masilahi na mshahara tayari wameyaweka sawa bado kusaini tu,” kilieleza chanzo chetu.

Kwa mara ya kwanza Kichuya alijiunga na Simba mwaka 2016 akitokea Mtibwa aliopocheza kwa mafanikio hadi mwaka 2018 alikotimkia Pharco ya Misri alikoshindwa kuwaka na kurejea Simba msimu 2020 lakini napo hakupata nafasi ya kucheza na sasa yupo Namungo.

KUHUSU MAJEMBE MAPYA YANGA…SURE BOY ATIKISA KICHWA ..KISHA AKAFUNGUKA HAYA…AIKUMBUKA AZAM FC … WALE WAZEE WA ‘HIZI KAZI’ DStv BAADA YA JANA KUWALETEA MAN UTD vs LIVER….MZIGO MWINGINE HUU HAPA…NI MSELELEKO TU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply