Habari za michezo

KAPOMBE AKIRI MAMBO MAGUMU SIMBA…AFUNGUKA A-Z JINSI MSIMU ULIOISHA ULIVYOKUWA WA TABU KWAO…

admin July 15, 2022 3:35 pm


Beki wa Kulia Simba SC Shomari Salum Kapombe ametangaza uhakika wa kikosi cha Klabu hiyo kupambana vilivyo msimu ujao wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ na Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Simba SC ilimaliza msimu wa 2021/22 mikono mitupu, ikipoteza Ubingwa wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ huku ikiishia hatua ya Robo Fainali katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, kwa kufungwa kwa changamoto ya Penati na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Kapombe amesema msimu uliopita ulikua mgumu kwa upande wao, lakini Simba SC imepanga kupambana msimu ujao ili kurejesha heshima yake iliyopotea.

“Msimu uliopita haukuwa mzuri kwetu, tulipoteza kila kitu, ilituumiza sana kwa kweli, lakini msimu ujao tutapambana ili kurejesha heshima yetu,”

“Tunamini timu yetu msimu ujao itakua Bora kwa sababu Uongozi umefahamu wapi tulipokosea, Mashabiki wanapaswa kuwa na imani  na timu yao, kwa hakika hatutawaangusha.” Amesema Kapombe

Simba SC ilikua inatetea Ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya tano mfululizo, Kombe la Shirikisho mara ya tatu mfululizo, lakini mipango hiyo iliishia mikononi mwa watani zao wa jadi Young Africans ambao walifaidika na Ubingwa wa michuano hiyo kwa msimu wa 2021/22.

BAADA YA MAN UTD KUIKAPAKUCHUA LIVERPOOL JUZI..LEO NI ZAMU YA CHELSEA…MZIGO WOTE NI MULE MULE NDANI YA DStv… KUHUSU HATMA YA KAGERE MSIMBAZI KWA MSIMU UJAO….AHMED ALLY AFUNGUKA NAMNA MAKUBALIANO YALIVYO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply