Habari za michezo

KUHUSU HATMA YA KAGERE MSIMBAZI KWA MSIMU UJAO….AHMED ALLY AFUNGUKA NAMNA MAKUBALIANO YALIVYO…

admin July 15, 2022 3:45 pm


Msemaji wa Simba SC, Ahmed Ally amesema straika wao Meddie Kagere bado ana mkataba na Wekundu hao hivyo ataendelea kuwepo.

Ahmed amesema, Kifaru huyo wa Rwanda bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Simba na ndio maana ameambatana na kikosi kilichoondoka leo nchini kuelekea Misri.

“Kagere bado yupo kwa mwaka Zaidi ndani ya Simba. Hivyo tutakuwa naye kwa msimu unaokuja,” alisema Ahmed.

Simba wameondoka nchini leo Julai 14, 2022 kuelekea Misri ambapo watakaa pre season kwa takriban wiki tatu kisha kurejea nchini kuanza msimu mpya wa 2022-23.

KAPOMBE AKIRI MAMBO MAGUMU SIMBA…AFUNGUKA A-Z JINSI MSIMU ULIOISHA ULIVYOKUWA WA TABU KWAO… BAADA YA WAARABU KUAMRIWA KUMLIPA FIDIA YA BIL1.6 ..MSUVA AWAPA SHARTI HILI GUMU…WAKIZINGUA FIFA INAWACHORA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply