Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama, amesema yeye pamoja na wachezaji wenzake, wanafahamu walipokosea msimu uliopita hivyo wanakwenda kujifua msimu ujao waweze kurejesha heshima yao.
Chama amefunguka hayo juzi Julai 14, 2022 akiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa ajili ya kuelekea nchini Misri kwa ajili ya maandalizi (pre season) ya msimu ujao wa ligi.
Amesema, anafahamu Simba ni timu kubwa na anafahamu mashabiki wanahitaji nini kutoka kwao hivyo kama wachezaji, wanakwenda kujifua ili wakirejea wawe fiti.
โNimeona timu zimesajili vizuri hasa hizi timu mbili kubwa Simba na Yanga, nawatakia kila lakheri wachezaji waliokuja, nina Imani wataongeza kitu kwenye ligi na wakiongeza itachochea pia wachezaji wengine kuja,โ alisema Chama.