Habari za michezo

JAMA JAMA HAWA DODOMA JIJI NAO WAPO POA KWENYE USAJILI…WASHUSA STRAIKA HILI LA MAANA…

admin July 20, 2022 8:00 am


Dodoma Jiji imeendelea kutikisa soko la usajili baada ya kumtambulisha rasmi Striker wa Kagera Sugar, Hassan Mwaterema.

Mbali na kucheza Striker Mwaterema pia hucheza winga na kabla ya kutua Kagera Sugar aliichezea JKT Tanzania.

Mwaterema anapishana na Striker wa Dodoma Jiji, Anuary Jabir ambaye tayari amemalizana  na ‘Wanankurukumbi’Kagera Sugar.

Mpaka sasa Dodoma Jiji imekamilisha usajili wa wachezaji  Daniel Mgore, Collins Opare na Christian Zigah kutoka Biashara United.

Wachezaji wengine waliotambulishwa na timu hiyo  ni Randy Bangala (TP Les Croyant) Amani Kyata,Rashid Chambo  (Coastal Union), Peter Paul (Azam) na Jimmy Shoji (Mbeya Kwanza)

Ofisa Habari wa timu hiyo, Moses Mpunga amesema mchezaji huyo amesaini kandarasi ya miaka 2 kuwatumikia walima za zabibu  hao ambao msimu uliomalizika hawakuwa na matokeo mazuri.

BAADA  YA KUHAKIKISHIWA MABILIONI YAKE…HATIMAYE MSUVA APATA TIMU MPYA…ASEPA BONGO KIMYA KIMYA… MAYELE: KAMA NILIWAFUNGA SIMBA NIKIWA SIJAFANYA MAZOEZI YA KUTOSHA….SAFARI HII LAZIMA WAITE MAJI MMAA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply