Home Geita Gold FC BAADA YA YANGA KUJAA MASTAA WA KAZI KAZI…YACOUBA SOGNE ACHONGEWA MCHONGO WA...

BAADA YA YANGA KUJAA MASTAA WA KAZI KAZI…YACOUBA SOGNE ACHONGEWA MCHONGO WA KUTUA GEITA GOLD…


Siku moja baada ya Yanga kutangaza kuwa kwenye mazungumzo ya kuachana na straika Yacouba Sogne, uongozi wa Geita Gold umeibuka na kutamka kuwa ni suala la muda kumtambulisha mchezaji huyo.

Yanga jana walitangaza kuachana na Chico Ushindi huku wakiweka wazi kuwa watakuwa na mazungumzo ya Yacouba ambaye Geita Gold tayari wametuma maombi ya kumuhitaji kwaajili ya kuongeza nguvu kikosini.

Akizungumza Mwenyekiti wa Bodi ya timu hiyo, Constantine Morandi alisema suala la kumalizana Yacouba lipo kwenye hatua nzuri huku akithibitisha mazungumzo ya mchezaji huyo ni baina yao na Yanga.

“Tulishapeleka barua ya kumuomba Yacouba na tuliambiwa tusubiri atakaporejea kutoka mapumziko ili tuweze kumalizana nao nazani kama mlivyosikia Yanga wakisema kuna mazungumzo basi ni baina yetu sisi Geita, mchezaji na waajiri wake wa zamani.”

Wakati huo huo Morandi alisema tayari wamekamilisha usajili wa wachezaji watano hadi sasa.

“Tumesajili beki wa kulia, kushoto beki wa kati, kiungo mshambuliaji wawili ni wachezaji wa kigeni kutoka Cameroon na Congo lengo kubwa la kuchanganya na wageni ni kuhakikisha tunafanya vizuri ndani na nje,” alisema na kuongeza;

“Tuna kila sababu ya kufanya maboresho kwenye kikosi chetu ambacho kinahitaji wachezaji wenye uzoefu wa kutosha ili kuonyesha chachu kwenye ligi ya ndani na mashindano ya kimataifa,” alisema.

Hadi sasa Geita imesajili nyota hawa Ramadhan Chombo (Biashara United), Yahya Mbegu (Polisi Tanzania), Haruna Shamte (Namungo),

Seleman Ibrahim ‘Boban’ (Mbeya City) na Hussein Bakari (Polisi Tanzania).

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA WAKIMTAMBULISHA CHAMA...MASAU BWIRE AIBUKA NA HILI KUHUSU RUVU SHOOTING YAKE...