Home Geita Gold FC WAKATI YANGA WAKIJICHIMBIA KIGAMBONI….GEITA GOLD WAIIZIDI MAARIFA….WAENDA NNJE YA NCHI KUWEKA KAMBI….

WAKATI YANGA WAKIJICHIMBIA KIGAMBONI….GEITA GOLD WAIIZIDI MAARIFA….WAENDA NNJE YA NCHI KUWEKA KAMBI….


Kocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Felix ‘Minziro’ leo anatarajia kuliongoza jeshi lake kuelekea Burundi tayari kwa maandalizi msimu mpya wa ligi na mashindano ya kimataifa.

Minziro ambaye alikuwa anatajwa kuachwa na timu hilo imethibitika kuwa wamemalizana na uongozi kwa mkataba wa miaka miwili ya kuendelea kukinoa kikosi hicho kinachojiandaa na mashindano ya Kombe la Shirikisho la Afrika na ligi.

Akizungumza Mwenyekiti wa bodi ya timu, Constantine Morandi alisema kwa upande wao kama viongozi wamekamilisha kilakitu kilichokuwa kinahitajika kutoka kwao sasa timu wameikabidhi kwa Minziro.

“Tulimpa ofa ya kuendelea kubaki na sisi ameikubali amesaini mkataba wa miaka miwili hivyo kesho (leo) ataongozana na timu kuelekea Burundi tayari kwa maandalizi tunatarajia mambo mazuri kutoka kwake na ingizo jipya la usajili,” alisema na kuongeza;

“Tumeongeza umakini katika dirisha la usajili hatutaki kurudia makosa kama tuliyoyafanya msimu ulioisha kwa kushindwa kufikia makubaliano na aliyekuwa kocha wetu aliyechukua hatua ya kutushtaki FIFA, usajili tulioufanya tutatambulisha wachezaji kwa kufuata sheria.”

Morandi alisema mashabiki wa Geita watarajie mambo mazuri kutoka kwao hasa katika usajili walioufanya kwani wanaamini utakuwa na chachu ya mafanikio kutokana na uzoefu wa waliowasajili kutoka ndani na nje.

Alisema Geita ina michuano mikubwa ambayo kwa upande wao ni msimu wao wa kwanza kushiriki wanahitaji maandalizi ya nguvu na ya kutosha kuhakikisha wanaiwakilisha vyema nchi na kuingia kwenye rekodi nzuri ya kushiriki kwa mara ya kwanza na kufanya vizuri.

SOMA NA HII  NABI ATANGAZA HALI YA HATARI...SILAHA ZA KUTISHA ZAIDI ZANOLEWA...ISHU NZIMA IKO HIVI