Simba SC wamecheza mechi ya kirafiki dhidi ya Abo Hamad ya mjini Ismailia ambapo wamemtandika bao 6 kwa bila.
Mchezo huo umepigwa jana ikiwa ni mwendelezo wa mechi za kirafiki ambazo kocha Zoran Maki anaendelea kuwapima wachezaji wake akiwa ameweka kambi ya wiki tatu mjini humo kabla ya kurejea jijini Dar kuanza Ligi Kuu msimu wa 2022-23.
Magoli hayo yamefungwa na Moses Phiri aliyepewa asist na Clatous Chama dakika 44 ya mchezo ambapo hadi mapumziko, Simba walitoka 1-0.
Kipindi cha pili kilipoanza, walitoka Moses Phiri, Victor Akpan, Henock Inonga, Chama na Habib Kyombo wakaingia Erasto Nyoni, Jimmyson, Outtara, Banda na Chris Mugalu.
Bao la pili lilipatikana dakika ya 57 likiwekwa kimyani na Jonas Mkude akipewa pasi na Okrah.
Dakika 59 ya mchezo walitoka Gadiel, Mkude na Okrah, wakaingia Taddeo, Kapama, Sakho na Kagere ambaye alitupia bao la tatu akipewa basi nzuri na Banda.
Goli la nne na la tano alifunga Sakho dakika 71 na 86 na Erasto Nyoni alimalizia la mwisho dakika ya 90 ya mchezo.