Habari za michezo

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA QATAR…ITV NA BBC ZAPIGANA VIKUMBO KUITAKA SAINI YA ‘KIBONGE’ WAYNE ROONEY…

admin July 25, 2022 6:00 pm


Huenda mkongwe wa soka kutokea England, Wayne Rooney akalazimika kukaa mbali na familia yake kwa kipindi kirefu zaidi baada ya tetesi kuwa yuko kwenye mazungumzo ya kazi nyingine ya mwishoni mwa mwaka.

Kwa mujibu wa Sunsport kampuni za ITV na BBC zimo katikati ya mchuano mkali wa kumpatia mshambuliaji huyo mkataba wa kuwa mtoa maoni/mchambuzi wa timu ya taifa ya England kwenye mashindano ya kombe la dunia 2022 nchini Qatar.

Hivi sasa Rooney amehamia Marekani ambako anaiongoza DC United na msimu wao wa sasa utafikia mwisho mnamo mwezi Oktoba hivyo kumpa muda mzuri kuweza kwenda Qatar kufanya kazi.

SAKATA LA KUFUNGIWA NA TFF….AFANDE SELE AMVAA MANARA…ADAI ANATABIA ZA KIPOPO…”TUMTETEE APIGE HELA ZAKE”… IKIWA NDIO MARA YAO YA KWANZA…GEITA GOLD WAPEWA RAMANI YA KUTIKISA MICHUANO YA CAF MSIMU UJAO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply