Habari za michezo

WAKATI WENZAO WAKIWA WASHANZA KAMBI NA MAANDALIZI YA MSIMU UJAO..NAMUNGO FC WAVUTANA WAO KWA WAO…

admin July 25, 2022 4:09 pm


Licha ya kuwepo kwa taarifa za kutaka kuweka kambi nje ya nchi, Uongozi wa Namungo umefunguka kuwa bado hawajafika muafaka wa wapi ambapo wataenda kuweka kambi kwa ajili ya msimu ujao.

Kikosi hicho kilichoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kwa msimu uliopita kilianza kambi tangu Julai 18 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Namungo, Hassan Zidadu amesema kuwa hadi sasa bado hawajapata muafaka wa sehemu gani wataweka kambi kwa ajili ya msimu ujao.

“Kwanza tulifikiria kuipeleka timu Kigamboni ama la! na baadae tukawaza kuipeleka nje ya nchi huko Zambia, lakini bado tamati ya mjadala huu lakini tukiamua wapi patatufaa basi tutaweka wazi.”

KISA TUZO YA SAKHO….MABOSI SIMBA ‘WAVIMBA MASHAVU’…WATUMA UJUMBE KWA YANGA… BAADA YA KMC KUMUONA WA NINI….MTIBWA SUGAR WAMBEBA JUMLA JUMLA SHIKALO…WAMFICHA TURIANI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply