Home Habari za michezo KISA MORRISON…MECK MEXIME APELEKA UBINGWA WA LIGI KUU KWA MARA NYINGINE JANGWANI…

KISA MORRISON…MECK MEXIME APELEKA UBINGWA WA LIGI KUU KWA MARA NYINGINE JANGWANI…


Kocha Mkuu wa Kituo cha Kulea na Kukuza vipaji vya soka kwa Vijana ‘Cambiaso Sports’ Meck Mexime, ameupa ‘TANO’ usajili wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, kuelekea msimu wa 2022/23.

Mexime amepongeza usajili huo, kwa kuamini Young Africans bado ina nafasi kubwa ya kutetea mataji yake msimu ujao, kutokana na wachezaji waliosajiliwa kuwa na uwezo wa kuendelea kuipambania Klabu hiyo ya Jangwani.

Amesema Viongozi wa Young Africans walijitathmini na kuona umuhimu wa kufuata ushauri wa kitaalamu uliotolewa na Benchi la Ufundi, na moja kwa moja ukaingia sokoni kusajili wachezaji wenye viwango na sifa za kupambana.

“Huwezi kuubeza usajili wa Young Africans kama unaakili timamu. Klabu ya Young Africans imefanya usajili wa kimbinu kuzingatia zaidi uweledi na sio ushamba kuonekana unajaza Wachezaji wasio na faida”

“Watazame Young Africans kwa jicho la tatu utagundua kwanza wamepitisha panga hasa kwa kuwatoa wachezaji wasioendana na falsafa ya mwalimu (Kocha), pia wachezaji wengine walikuwa mizigo tu kwa klabu bila sababu” amesema Mexime

Young Africans imesajili wachezaji watano wa Kimataifa ambao ni Lazarius Kambole (Zambia), Bernard Morrison (Ghana), Gael Bigirimana (Burundi), Joyce Lomalisa (DR Congo) na Stephen Aziz Ki (Burkina Fasso).

Wachezaji walioachwa ni Deus Kaseke, Paul Godfrey ‘Boxer’, Yassin Mustapher (Tanzania) na Chiko Ushindi (DR Congo).

SOMA NA HII  KWA FUJO HIZI MSIMU UJAO BINGWA NI AZAM FC AISEE....LOMALISA NAYE HUYOO CHAMAZI....