Home BIashara United RASMI….SIMBA KUWAPITISHIA FAGIO LA CHUMA MUGALU NA KAGERE…ISHU YA MANZOKI SAWA NA...

RASMI….SIMBA KUWAPITISHIA FAGIO LA CHUMA MUGALU NA KAGERE…ISHU YA MANZOKI SAWA NA PUA NA MDOMO…


Tetesi tulizozipata kutoka Klabu ya Simba ni kuwa, washambuliaji wa timu hiyo Meddie Kagere raia wa Rwanda na Chris Mugalu raia wa Congo DR wako kwenye mazungumzo ya kuvunja mkataba.

Inaelezwa kuwa, mpaka sasa miamba hao wa kufumania nyavu ambao wamebakiza mkataba wa mwaka mmoja mmoja kila mmoja ndani ya Simba bado wako kikosini katika kambi ya Simba nchini Misri huku majadiliano yakiendelea.

Taarifa za ndani kutoka kwenye klabu hiyo zinadai kuwa Mugalu na Kagere ambao hawakuwa na wakati mzuri sana msimu uliopita inaelezwa imekuwa ngumu kufikia makubaliano ya kuachana na Simba kwa sababu wametaka kulipwa pesa nyingi ili kuvunja mikataba yao.

Aidha, Kocha Zoran Maki ameuambia uongozi wa Simba SC kuwa anataka kuongezewa mshambuliaji mwngine mmoja na kiungo mshambuliaji mmoja huku lengo lake kubwa ikiwa ni kumnasa Manzoki wa Vippers ya Uganda.

Klabu ya Simba SC imetuma kiongozi nchini Uganda ???????? kufanya mazungumzo ya kumpata mshambuliaji Manzoki ambaye walipanga kumtumia Manzoki kwenye michuano ya kimataifa ya (CAF) ambaye timu yake imemng’ang’ania mpaka mkataba wake utakapomalizika Oktoba mwaka huu.

Iwapo Simba watasubiri dirisha dogo ili wampate bure, Manzoki atakuwa tayari ameshaitumikia Vippers, hivyo hatatumika kwenye michuano ya (CAF) iwapo atajiunga na Simba Sc kama ilivyokuwa kwa Chama msimu uliopita akitoka RS Berkane.

Bado mazungumzo ya kumnasa Manzoki yanaendelea lakini Vippers wamesema wanataka Tsh milioni 460 ili wamruhusu mchezaji huyo ajiunge Simba.

SOMA NA HII  BAADA YA TAARIFA ZA KUPEWA RUSHWA NA WALIBYA KUWA NYINGI..BIASHARA UTD WAIBUKA NA HILI...