Habari za michezo

AHMED ALLY : JEZI YA YANGA NI MBAYAAA MPAKA AIBU TUNAONA SISI…’KAF’ HAWAWEZI KUIKUBALI…

admin July 29, 2022 12:01 pm


Meneja wa Habari na Mawasilino wa Klabu ya Simba SC Ahmed Ally ameibeza Jezi mpya ya nyumbani ya Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans, baada ya kufanyiwa uzinduzi jana Alhamis (Julai 28), jijini Dar es salaam.

Young Africans ilizindua jezi tatu maalum za msimu ujao 2022/23 (Nyumbani, Ugenini na Chaguo la tatu), huku wengi wakisifia jezi hizo, na baadhi ya wadau wakibeza.

Ahmed Ally ametumia kurasa zake za mitandao ya Kijamii kubeza jezi ya nyumbani ya Young Africans ambayo imenakshiwa na mfano wa picha za baadhi ya alama maalum zilizopo kwenye mikoa ya Tanzania.

Ahmed ameandika: Nimevumilia nimeshindwa acha tu niseme NI MBAYAAA.

Vaa lakin ukijua kuwa umevaa kitu kibayaaaaa na ukivaa unanyata.

Na Sidhani kama KAF watakubali Uniform zenye miundombinu maana nimeona mpaka machinjio ya Vingunguti na Dampo la Kinyamwezi.

Ni mbayaa mpaka aibu tunaona sisi.

KUELEKEA MSIMU UJAO…MTIBWA SUGAR WAMALIZANA CHAP CHAP NA KIFAA MATAA CHA SIMBA SC… PAMOJA NA WOTE KUWA MISRI….SIMBA WAIPOTEZEA KIMTINDO AZAM FC…WADAI HAWANA ‘TIME’ NAO..KILA MTU AFE KIVYAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply