Habari za michezo

KIPIGO KUTOKA KWA WAARABU CHAMCHEFUA KOCHA MAKI….AWAPA MAKAVU LIVE MASTAA WAPYA…CHAMA AHUSISHWA…

admin July 30, 2022 9:47 am


BAADA ya  Jumatano kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Klabu ya Haras El Hadood ya Misri kwenye mchezo wa kirafiki wa maandalizi ya kabla ya msimu, Kocha Mkuu wa Simba, Zoran Manojlovic ‘Maki’, amewachimba mkwara viungo wa timu hiyo kuwa hajafurahishwa na ubora wa kutengeneza nafasi waliouonyesha katika mchezo huo na kuonya wanapaswa kubadilika.

Simba Jumatano walikubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Haras El Hadood katika mchezo huo wa kirafiki wa mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa 2022/23, huku mchezo huo ukiwa ni wa tatu  Simba tangu waanze kambi yao, ambapo katika michezo miwili iliyopita walishinda dhidi ya Abo Hamad na kutoa sare dhidi ya Ismailia.

Katika mchezo huo wa juzi dhidi ya Haras El Hadood Simba walianza na viungo watano ambao ni Pape Sakho, Moses Phiri, Peter Banda, Augustine Okrah, Clatous Chama na Jonas Mkude.

Akizungumzia mchezo huo, kocha Zoran alisema: “Tumefurahi kupata mchezo huu kwa kuwa umekuwa kipimo sahihi cha maendeleo ya kikosi chetu kabla ya kuanza kwa msimu mpya, hatukuwa bora hususan katika nafasi ya kiungo.

“Tulishindwa kabisa kutengeneza nafasi kama ambavyo ilitupasa na nadhani ni jambo ambalo lazima tuhakikishe tunalirekebisha.”

NDALA AANIKA ALIYOYAONA KAMBI YA AZAM NCHINI MISRI…ATOA ONYO KWA MASTAA WAPYA…. KUFUZU CHAN…STARS KUMALIZIA KAZI YA ‘KUSAFISHA JALALA LEO’…WAKIZINGUA NDIO BASI TENA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply