Burudani

BAADA YA KUCHAPWA TENA JANA…MANDONGA AIBUKA NA KALI HII MPYA…ADAI ALIPIGWA NGUMI MBILI AKAYUMBA KIDOGO…

admin July 31, 2022 12:57 pm


Baada ya kuchapwa kwa Technical Knock Out, Karim Mandonga ametoboa siri ya kipigo huku akiwaomba mashabiki wake kutorudi nyuma.

“Mpinzani wangu alinipiga right (ngumi ya kulia) akaunganisha na left hook, nikayumba, wakati natambalia mikono nikitaka  kunyanyuka refarii akamaliza pambano,” amesema Mandonga.

Amesema Mandonga mtu kazi yuko fiti na mashabiki wake wasirudi nyuma kwani kukosea leo sio kukosea kesho.

“Michezo yetu ni ya makosa, ukifanya kosa moja mwenzako tumia kukumaliza, ndicho kimetokea kwangu,” amesema.

Mandonga amechapwa kwa TKO na Shaban Kaoneka raundi ya nne ya pambano lililopigwa mjini Songea usiku wa kuamkia leo.

“Nilijitahidi sana kupambana, lakini jitihada zangu ziliishia pale, lakini matokeo yale hayatanirudisha nyuma, sasa nataka kuzichapa na watu wenye rekodi bora kwenye ngumi, hasa wakongwe.

“Nikirudi Dar es Salaam naenda kupiga kambi na mabondia wa Ngome nikajifue jeshini hivyo atajayefuata kazi anayo,” amesema.

Kuhusu tambo zake zilizomtambulisha zaidi kwenye ndondi,  Mandonga amesema kila mmoja Mungu kamuandaa na kumpa kipaji chake.

“Naamini mimi kaniandaa hivi na  nafsi yangu ilishakubali kupambana ,” amesema bondia huyo anayepigania uzani wa super middle.

BANGALA ARUDI YANGA NA MZUKA KAMA WOTEE…AKUTANISHWA NA GSM WAKUBALIANA MAMBO HAYA MAPYA… SIKU KADHAA BAADA YA YANGA KUZINDUA JEZI…SIMBA WAIBUKA NA KUTAMBA KUHUSU JEZI ZAO..WADAI ZINATOKA ULAYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply