Home Habar za Usajili Simba ACHANA NA UTAMBULISHO WA AKPAN LEO…MASTAA HAWA HAPA WANAFUATA KUTUA MSIMBAZI…HAKIKISHA UNABANDO…

ACHANA NA UTAMBULISHO WA AKPAN LEO…MASTAA HAWA HAPA WANAFUATA KUTUA MSIMBAZI…HAKIKISHA UNABANDO…


Klabu ya Simba imenasa saini ya kiungo Mnigeria, Victor Akpan kwa mkataba wa miaka miwili akitokea katika timu ya Coastal Union.

Nyota huyo aliyeonyesha kiwango kizuri msimu ulioisha unakuwa ni usajili wa pili kwa wachezaji wakigeni ndani ya timu hiyo baada ya hapo awali kutambulishwa Moses Phiri kutoka Zanaco ya Zambia.

Simba chini ya Kocha mpya, Zoran Maki inaendelea kuboresha kikosi chake kwa ajili ya michuano mbalimbali ya Ligi Kuu Bara na ile ya kimataifa huku hadi sasa ikinasa saini ya nyota kadhaa wakiwemo, Habib Kyombo kutoka Mbeya Kwanza na Nassoro Kapama aliyetokea Kagera Sugar.

Mbali na Usajili huo taarifa za kuaminika zinadai kuwa nyota wengine ambao wamejiunga na miamba hiyo ni mshambuliaji raia wa Uganda, Cesar Manzoki aliyetokea (Vipers FC), Nelson Okwa (Rivers United) na Augustine Okrah aliyetokea Asante Kotoko ya Ghana.

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA WAKIITAKA FAINALI YA SHIRIKISHO AFRIKA...PABLO KAWATAZAMA WEE..KISHA AKASEMA NUSU...