Home Azam FC BOSI AZAM FC AFUNGUKA WALIVYOHANGAISHWA KUPATA SAINI YA SOPU…AFUNGUKA A-Z SIMBA NA...

BOSI AZAM FC AFUNGUKA WALIVYOHANGAISHWA KUPATA SAINI YA SOPU…AFUNGUKA A-Z SIMBA NA YANGA ZILIVYOSUMBUA…


Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam FC, Abdulkarim ‘Popat’ amesema usajili wote walioufanya msimu huu ulikuwa ni mgumu kuukamilisha lakini kuzipata saini za mastaa wao Abdul Suleiman ‘Sopu’ kutoka Coastal Union na Kipre Junior aliyetoka Sol FC ya Ivory Coast, jasho liliwatoka.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Popat alisema ugumu kwa nyota hao ni kutokana na kugombewa na klabu mbalimbali hali iliyoongeza ushindani mkubwa ila jambo wanaloshukuru ni kufanikisha hilo kwa matakwa ya benchi lao la ufundi.

“Kwa Sopu timu nyingi na kubwa hapa Tanzania zilikuwa zikimtaka tena kwa ushawishi mkubwa lakini mwenyewe alionyesha mapenzi kwetu na tukamnasa, kwa Kipre kuna klabu za kwao Ivory Coastal na Ghana zilizomuhitaji hivyo ilikuwa ngumu sana,” alisema Popat.

Aliongeza usajili wao umezingatia zaidi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu ujao kwani ni muda mrefu kwao tangu walipoutwaa 2013/14. “Malengo yetu yapo palepale na hilo halijabadilika, ni kweli hatujachukua ubingwa kwa muda mrefu lakini kama mnavyofahamu Simba na Yanga ndio timu zilizojizatiti hivyo sio rahisi kuziangusha ila tupo kwenye njia sahihi ya mafanikio na tutafanikisha hilo,” alisema.

Waliosajiliwa ni Waivory Coast, Kipre na Tape Edinho, Mnigeria Isah Ndala, Nathaniel Chilambo, Cleophace Mkandala, Abdul Sopu, Mghana James Akaminko, Mcomoro Ali Ahamada na beki Msenegal Malickou Ndoye.

SOMA NA HII  KISA MATOKEO YA SARE JANA...AHMED ALLY AIITA YANGA 'WACHAWI UNITED'...ADAI WAMEFUKIA HIRIZI...