Home Habar za Usajili Simba ISHU YA MANZOKI KUTUA MSIMBAZI…NGOMA BADO NGUMU….VIPERS WAKOMAA WALIPWE MIL 450…SIMBA WACHOMOA…

ISHU YA MANZOKI KUTUA MSIMBAZI…NGOMA BADO NGUMU….VIPERS WAKOMAA WALIPWE MIL 450…SIMBA WACHOMOA…


Mashabiki wa Simba wanaendelea kuifuatilia timu hiyo ikiwa kambini Misri, huku wakimsikilizia straika mpya Cesar Manzoki, lakini Za Ndaani Kabisa zinasema, jamaa huenda akajiunga na kikosi hicho dirisha dogo linalofunguliwa Desemba mwaka huu.

Habari za Ndani zinasema, licha ya straika huyo kusainishwa mkataba, lakini mabosi wake wa zamani, Vipers ya Uganda wameleta ugumu kwa kutaka ilipwe Dola 200,000 (zaidi ya Sh450 milioni za miezi miwili iliyosalia za mkataba na mchezaji huyo raia wa Afrika ya Kati mwenye asili ya Congo.

Inaelezwa Vipers umekomaa mchezaji huyo amebakiza mkataba wa miezi miwili na kama Simba inamtaka basi ilipe fedha hizo, kitu ambacho mabosi wa Msimbazi wameona isiwe tabu, wanamwacha aendelee kukipiga Vipers, kisha wambebe Desemba kama Mchezaji Huru.

Manzoki tayari yupo na timu yake inayojiandaa na msimu mpya wa Ligi ya Uganda, huku Simba nao ikiwa Misri ikiendelea na maandalizi ya msimu mpya (pre-season’).

“Tunapambana kuona kama tunaweza kumpata kabla dirisha la usajili wa Caf halijafungwa Agosti 15 ikishindikana hapo basi itabidi tusubiri hadi dirisha dogo, tumchukue kama mchezaji huru.”

“Pesa wanayoitaka ni nyingi na mchezaji amebakiza mkataba wa miezi miwili, shida ipo hapo, wamekomaa walipwe Dola 200,000 ambayo ni pesa nyingi mno, ila ngoja tuone mazungumzo yatakavyoisha na ikishindikana basi tutamchukua Desemba,” alisema kiongozi huyo.

SOMA NA HII  HUYU HAPA DEJAN GEORGIJEVIC...MTAMBO WA MABAO SIMBA KUTOKA ULAYA....AAPA KULIPA KISASI CHA KUZOMEWA NA YANGA...