Home Habari za michezo KISA KUZOZANA NA KARIA….TFF WAMFUNGULIA SHAURI LA KESI MANARA…AKUMBUSHWA KANUNI ZA KUZINGATIA…

KISA KUZOZANA NA KARIA….TFF WAMFUNGULIA SHAURI LA KESI MANARA…AKUMBUSHWA KANUNI ZA KUZINGATIA…


Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefungua shauri mbele ya Kamati ya Maadili dhidi ya ofisa wa klabu ya Yanga, Haji Manara kutokana na vitendo vya ukiukaji wa maadili.

Kamati ya Maadili kupitia kwa Mwenyekiti wake tayari imepewa taarifa kuhusu malalamiko dhidi ya Manara, hivyo itapanga siku ya kusikiliza shauri hilo na Mlalamikiwa atapewa taarifa.

TFF inawakumbusha wanafamilia ya mpira wa miguu kuwa wanabanwa na Katiba na Kanuni mbalimbali za mchezo huo, hivyo wanatakiwa kuwa makini kwa vitendo na kauli zao kuhusu mpira wa miguu.

Taarifa hii imekuja baada ya jana kuonekana Haji Manara akizozana na Rais wa TFF Wallace Karia kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume, katika fainali ya ASFC 2022 kati ya Yanga na Coastal Union.

SOMA NA HII  KWA MARA NYINGINE TENA ..NIYONZIMA AFUNGUKA KUHUSU YANGA..ATOA ONYO KALI