Home Habar za Usajili Simba KUHUSU ISHU YA SADIO KANOUTE…SIMBA WAVUNJA UKIMYA KUHUSU JAMBO LAKE…PASSPOTI YAWA KIKWAZO…

KUHUSU ISHU YA SADIO KANOUTE…SIMBA WAVUNJA UKIMYA KUHUSU JAMBO LAKE…PASSPOTI YAWA KIKWAZO…


Baada ya kuwepo na maswali mengi kuhusu alipo kiungo wa Simba SC, Sadio Kanoute, msemaji wa klabu hiyo ameibuka na kutoa ufafanuzi kupitia ukurasa wake wa Instagram.

“Yuko wapi Sadio Kanoute mbona hatumuoni Pre Season??! Kanoute alirejea kwao Mali kwa ajili ya kubadilisha Hati yake ya kusafiria (Passport) ambayo imekaribia kujaa.

Lakini kumekua na changamoto ya kupata Passport mpya kwa wakati na haraka kutokana na hali ya mambo nchini mwao. Leo amerejea Dar es Salaam na ameanza taratibu za kuja Misri kujiunga na wenzie.”

SOMA NA HII  HUYU AZIZI KI MNAEMUONA NI ASILIMIA 40 TU