Home Habari za michezo KUHUSU MAANDALIZI YA MSIMU UJAO…HIVI NDIVYO DODOMA JIJI WALIVYOIZIDI KETE YANGA...

KUHUSU MAANDALIZI YA MSIMU UJAO…HIVI NDIVYO DODOMA JIJI WALIVYOIZIDI KETE YANGA YA BILIONEA GSM…


Wakati Yanga wakiamua kuifanya kambi yao ya maandalizi ya msimu ujao hapa Dar esSalaam, timu ya Dodoma Jiji imeanza maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu na leo Julai 21 imeenda jijini Arusha kuweka kambi  huku ikiachana na wachezaji 13 akiwemo Khamis Mcha ‘Vialli’ na Issa Abushehe.

Timu hiyo ilianza mazoezi  jana na leo imeendelea nayo  katika uwanja wa Jamhuri jijini hapa ambapo wachezaji kadhaa wapya na wale wa zamani walionekana.

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Mosses Mpunga amesema sababu ya kuweka kambi Jijini  Arusha ni kutokana na jiji hilo  kuwa na mazingira ya utulivu.

Mpunga amesema Arusha watakaa kwa siku kadhaa na kisha wataelekea sehemu nyingine ambayo bado uongozi haijaitaja  kwa ajili ya kuendeleza kambi hiyo.

Wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo na walionekana mazoezi ni pamoja  Randy Bangala (TP Les Croyant) Amani Kyata,Rashid Chambo  (Coastal Union)  Jimmy Shoji (Mbeya Kwanza) na Hassan Mwaterema (Kagera Sugar)

Wachezaji wa zamani walionekana mazoezini ni pamoja na nahodha,Mbwana Kibacha,Rajabu Mgalula,Augustino Nsata,Salmin Hoza,Emmanuel Martin,Joram Mgeveke,Seif Karihe na enrick Nkosi.

Mazoezi hayo yalisimamiwa na Kocha Masoud Djuma na msaidizi wake Mohammed Muya.

Mcha Abushehe watupiwa virago

Katika hatua nyingine inadaiwa uongozi wa klabu hiyo umewaacha baadhi ya wachezaji akiwemo Issa Abushehe na Khamis Mcha.

Mcha ambaye ameitumikia klabu hiyo kwa miaka minne  alikuwa nahodha msaidizi kwenye kikosi hicho na  msimu uliopita aliifungia  mabao matano  huku matatu akifunga kwa  njia ya   penalti.

Aliyeongoza ufungaji katika kikosi cha timu hiyo  ni Anuary Jabir  aliyefunga mabao saba huku Mcha akishika nafasi ya pili kwa mabao yake matano.

Abushehe ambaye ameifungia bao moja timu hiyo  alijiunga dirisha dogo la usajili akitokea Coastal Union ya Tanga na alikosa mechi saba za mwisho kutokana na kuumia.

Uongozi wa timu hiyo bado haujaweka wazi majina ya wachezaji iliyowaacha  lakini Mwansporti   inajua  wachezaji hao wametupiwa virago kwani kwenye mazoezi ya jana na leo  hawakuonekana.

SOMA NA HII  KISA MAFANIKO YA YANGA CAF...WAKUU WA MIKOA WANYUKANA UKUMBINI...UBISHI ULIANZA HIVI...

Wachezaji wengine ambao hawakuonekana mazoezini ni pamoja na  Justin Mganga Daga Chenko,Omary Kanyoro,Makipa Yusuphu Mohammed  Rahim Sheike na Hussein Msalanga ambaye inadaiwa tayari amejiunga na Ruvu Shooting.

Alipotafutwa Mcha amesema yupo safarini hawezi kuzungumza kitu chochote.

Kwa upande wake Abushehe amesema tayari ameachana na timu hiyo na jana aliwaaga viongozi,benchi la ufundi  na wachezaji wa timu hiyo.