Home Habari za michezo TUZO ZA CAF: SAKHO AIPEPERUSHA BENDERA YA SIMBA ….ABEBA TUZO YA GOLI...

TUZO ZA CAF: SAKHO AIPEPERUSHA BENDERA YA SIMBA ….ABEBA TUZO YA GOLI BORA LA MWAKA KIBABE….MANE AMPIGIA SALUT..


Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba, Pape Ousmane Sakho ameshinda tuzo ya bao bora la mwaka, alilofunga kwenye mchezo wa hatua ya makundi kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya ASEC Mimosa.

Wakati akiinuka kwenda kupokea tuzo hio, Sakho alikumbatiwa kwa dakika kadhaa na Mshambuliaji hatari wa Senegal na klabu ya Bayern Munich, Sadio Mane, pamoja na kocha wa timu ya taifa ya Senegal.

Katika orodha ya mwisho iliyotolewa jana na CAF baada ya mchujo wa kupunguza idadi ya wanaowania tuzo hizo, Sakho amebaki katika kinyang’anyiro cha goli bora la mwaka akiwa sambamba na Gabadinho Mhango wa Malawi na Orlando Pirates pamoja na Zouhair El Moutaraji wa Morocco na klabu ya Wydad Casablanca.

Kiungo huyo mshambuliaji wa Simba, amewapiku Adama Congo (Burkina Faso), Ben Malango (DR Congo), Ellyes Skhiri (Tunisia), Haithem Layouni (Tunisia), Keitumetse Dithebe (Botswana), Sanaa Massoudy (Morocco) na Youssouf M’Changama (Comoro).

Sakho alifunga bao hilo kwa staili ya tiktak akiunganisha kwa mguu wa kulia krosi iliyopigwa na beki wa Simba, Shomari Kapombe aliyepokea mpira uliotokana na kona fupi iliyochongwa na Rally Bwalya.

SOMA NA HII  MASOUD DJUMA AANZA KUTOA SABABU DODOMA JIJI...ANADAI HAIPENDI TIMU....AITAJA SIMBA SC..