Home Habari za michezo MIDO WA NEWCASTLE YA UINGEREZA ATAMBULISHWA YANGA… UKUMBI WALIPUKA KWA SHANGWE…

MIDO WA NEWCASTLE YA UINGEREZA ATAMBULISHWA YANGA… UKUMBI WALIPUKA KWA SHANGWE…


RAIS mteule wa klabu ya Yanga, Hersi Said amemtambulisha rasmi kiungo aliyewahi kucheza Newcastle United ya Uingereza, Gael Bigirimana katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere unapofanyika uchaguzi wa timu hiyo.

Akizungumza mbele ya wajumbe, Hersi amesema mchezaji huyo ana sifa kubwa kwani amecheza katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Hersi amesema wao wanasajili wachezaji wazuri na ndio maana wamemchukua mchezaji  wa zamani wa klabu ya Newcastle iliyokuwa inashiriki Ligi Kuu nchini Uingereza.

“Sisi tunasajili na tumeahidi kabisa kushusha vifaa, huyu hajacheza timu ndogo bali amecheza timu kubwa na kwenye Ligi Kubwa,” amesema Hersi na kuongeza;

“Wanasema eti Mayele ataenda Kaizer Chiefs, sisi wenyewe tunachukua wachezaji kwao huko.”

Hersi amesema wamefanya usajili wa wachezaji watano wa nguvu na watendelea kuwatambulisha mpaka wanamaliza.

“Kuna mchezaji tutamtambulisha leo usiku saa tisa, mwingine ataingia Jumatatu, huyu wa Jumatatu amecheza Ligi ya Spain,” amesema Hersi.

Yanga mpaka sasa imewatambulisha rasmi, Lazarous Kambole, Benard Morrison na Gael Bigirimana.

SOMA NA HII  AZAM: 'UNBEATEN' YA YANGA ILILINDWA SANA NA WAAMUZI...