Home Habari za michezo RASMI….MATAJIRI WAPYA LIGI KUU WAMALIZANA NA DEUS KASEKE JUMLA JUMLA…

RASMI….MATAJIRI WAPYA LIGI KUU WAMALIZANA NA DEUS KASEKE JUMLA JUMLA…


KLABU ya Singida Big Stars imetangaza rasmi kunasa saini ya aliyekuwa kiungo wa Yanga, Deus Kaseke kwa mkataba wa miaka miwili.

Kaseke aliachana na Yanga Julai 14 mwaka huu baada ya mkataba wake na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara Yanga kufikia ukomo.

Nyota huyo aliyejiunga na Yanga kwa mara ya kwanza mwaka 2015 alishindwa kuongezewa mkataba mpya kutokana na kushindwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara chini ya Kocha mkuu Nasreddine Nabi huku akicheza zaidi akitokea benchi.

Kaseke ambaye ameitumikia Mbeya City na Singida United anakuwa mchezaji wa tatu kutoka Yanga kujiunga na timu hiyo baada ya awali kutangazwa mabeki, Paul Godfrey ‘Boxer’ na Yassin Mustapha ambao nao walitemwa.

Mbali na mastaa hao ila Kaseke anaungana na Kelvin Sabato aliyetoka Mtibwa Sugar, Metacha Mnata (Polisi Tanzania), Abdulmajid Mangalo (Biashara United), Said Ndemla (Mtibwa Sugar) na Benedict Haule wa (Azam FC).

SOMA NA HII  SASA NI RASMI FAINALI ITAKUWA SIMBA V YANGA, KIGOMA