Home news SASA NI RASMI FAINALI ITAKUWA SIMBA V YANGA, KIGOMA

SASA NI RASMI FAINALI ITAKUWA SIMBA V YANGA, KIGOMA


 SIMBA ikiwa imetwaa taji la Kombe la Shirikisho mara mbili inakwenda kukutana na Yanga iliyotwaa taji hilo mara moja katika mchezo wa fainali unaotarajiwa kuchezwa Kigoma.

Mchezo wa leo Juni 26 ambao ulikuwa ni wa nguvu kubwa na akili nyingi ulishuhudia Simba ikipachika bao la ushindi dk 89 kupitia kwa Luis Miquissone aliyetumia pasi ya Bernard Morrison.

Ni bao hilo liliibua utata kwa wachezaji wa Azam FC wakiongozwa na nahodha Agrey Morris ambao walionekana wakimzoga mwamuzi wa mchezo huo kwa kile walichokuwa wakionekana kulalamika Morrison kuanzisha mpira kwa haraka.

Licha ya wachezaji kulalamika na kuonyeshwa kadi za njano ikiwa ni kwa Bruce Kangwa bado mwamuzi aliweka mpira kati na ngoma ikakamilika Azam FC 0-1 Simba, Uwanja wa Majimaji.

Ushindi huo unaifanya Simba kuifuata hatua ya fainali Yanga ambayo jana ilishinda bao 1-0 dhidi ya Biashara United katika nusu fainali ya kwanza.

SOMA NA HII  GOMES AMUAMULIA MKUDE...AMBADILISHA NAMBA..SASA KUCHEZA PACHA NA 'VARANE'