Home Habari za michezo TULISEMA NA IMETOKEA….KUELEKEA MSIMU UJAO..KAPAMA NI MNYAMA…VYUMA VINGINE VINAVYOSUBIRIWA NI HIVI…

TULISEMA NA IMETOKEA….KUELEKEA MSIMU UJAO..KAPAMA NI MNYAMA…VYUMA VINGINE VINAVYOSUBIRIWA NI HIVI…


KLABU ya Simba imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo nyota Nassoro Kapama kutoka Kagera Sugar kwa mkataba wa miaka miwili.

Usajili wa mchezaji huyu ni miongoni mwa taarifa za awali ambazo Soka la Bongo tuliziandika kuwa muda wowote angeweza kutangazwa kujiunga na wekundu hao wa msimbazi.

Kapama ana uwezo wa kucheza nafasi nyingi ndani ya kiwanja ikiwemo beki, kiungo na nafasi ya ushambuliaji hali iliyowavutia benchi la ufundi la Simba.

Kwa msimu uliopita Kapama akiwa Kagera Sugar amecheza mechi 25, akifunga mabao mawili na kutoa usaidizi wa magoli 3 (assist tatu)

Simba imeendelea kuimarisha safu yao ya kiungo kuelekea msimu mpya wa mashindano, wekundu hao wa msimbazi inatarajiwa kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika.

Mbali na Usajili huo taarifa za kuaminika zinadai kuwa nyota wengine ambao wamejiunga na miamba hiyo ni mshambuliaji raia wa Uganda, Cesar Manzoki aliyetokea (Vipers FC), Nelson Okwa (Rivers United) na Augustine Okrah aliyetokea Asante Kotoko ya Ghana.

SOMA NA HII  NABI ASHTUKIA MCHEZO MCHAFU YANGA...AIGA MBINU ZA SVEN ..SASA NI MWENDO WA SHOW SHOW....