Home Habari za michezo WAKATI MADRID WAKITAKA KUMSAJILI RONALDO…MASHABIKI WAIBUKA NA KAMPENI YA KUMKATAA…

WAKATI MADRID WAKITAKA KUMSAJILI RONALDO…MASHABIKI WAIBUKA NA KAMPENI YA KUMKATAA…


Mashabiki wa klabu ya Atletico Madrid wameanzisha kampeni kwenye mitandao ya kijamii kushinikiza klabu yao kutokumsajili mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Cristiano Ronaldo.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa mwenye umri wa miaka 37, mwishoni mwa mwezi June, aliwasilisha ombi la kutaka kuaondoka kwenye klabu ya Man Utd licha kubakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake.

Awali, klabu za Chelsea na FC Bayern ziliripotiwa kuhitaji huduma ya mshambuliaji huyo kabla kujiondoa kwenye kinyanganyiro hicho.

Taarifa kutoka nchini Hispania zinasema kuwa klabu ya Atletico Madrid inahitaji huduma ya mshambuluaji huyo na wako tayari kumuweka sokoni Antoine Griezmann ili kuweza kupunguza bill ya mshahara kwa ajili kufanikisha usajili wa Ronaldo.

Mashabiki wa Atletico Madrid hawataki klabu yao imsaini mchezaji huyo, ambaye alikuwa mchezaji wa wapinzani wao Real Madrid.

Mashabiki wameanzisha kampeni ambayo wameipa jina ‘#ContraCR7’ ikiwa na maana ya kumkataa mchezaji huyo

SOMA NA HII  A-Z YANGA WALIVYOIFANYIA KITU MBAYA NAMUNGO JANA....NSAJIGWA AFUNGUKA MCHEZO MZIMA...