Home Habari za michezo DILI LA MAYELE KUTUA AFRIKA KUSIN LAMFIKIA ‘PROFESA’ NABI…NA HAYA NDIO MAJIBU...

DILI LA MAYELE KUTUA AFRIKA KUSIN LAMFIKIA ‘PROFESA’ NABI…NA HAYA NDIO MAJIBU YAKE….


Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amerejea nchini kuanza maandalizi ya msimu, huku akimaliza utata kwa kutoa taarifa kwa mashabiki kuwa straika Fiston Mayele; “haondoki”

Awali kulikuwa na sintofahamu juu ya Mayele, aliyekuwa akitajwa kutakiwa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na Al Hilal ya Sudan, lakini Nabi alisema amezungumza na nyota huyo aliyekuwa kinara wa mabao wa timu hiyo na kwamba yupo sana tu kikosini.

Nabi amesema alilazimika kufanya kikao na Mayele kwa njia ya simu wakati wote wakiwa makwao kwa mapumziko juu ya uvumi kwamba anataka kugoma kurejea Yanga kwa msimu ujao. “Ni kweli Mayele ana mkataba halali na Yanga uliosalia mwaka mmoja, lakini shida ni ofa ambazo Al Hilal na Kaizer Chiefs na hasa hawa Wasudan.”

“Fedha walizomuahidi zingemchanganya yeyote bila kujali hata kama bado uamuzi ulitakiwa kutolewa na klabu juu ya kumuuza au la. Nafahamu klabu tulishatoa msimamo hakuna mchezaji tunayemhitaji ataweza kuondoka kwa sasa, kwani tuna malengo makubwa msimu ujao.”

Nabi alisema katika mazungumzo yake na Mayele aliyemaliza na mabao 16 na kushika nafasi ya pili nyuma ya kinara wa Ligi Kuu, George Mpole wa Geita Gold aliyefunga 17, mshambuliaji huyo amekubali kusalia Yanga kwa msimu ujao ili kumalizia mkataba wake.

“Kuna mambo mengi yaliharibu saikolojia yake, sote tunafahamu Mayele alitakiwa kuwa mfungaji bora msimu uliopita, kila mmoja katika timu viongozi, sisi makocha, wachezaji wenzake na hata mashabiki wa Yanga waliumizwa na lililotokea mwishoni mwa msimu.

“Nimeongea naye na amekubali kubaki hapa kwa kumalizia mwaka wake, pia kama atakubali kubaki zaidi hapa, huyu ni mchezaji kati ya wale waliotupa thamani kubwa, sio kila timu inaweza kuwa na mtu bora kama Mayele,” alifafanua Nabi.

Alisema kubaki kwa Mayele atakayewasili kesho Jumamosi kutaiongezea nguvu kwani yupo Lazarous Kambole na Stephane Aziz KI sambamba na kiungo Gael Bigirimana na beki Joyce Lomalisa.

“Tulihitaji kuwa na timu bora ambayo itakwenda kutupa thamani kimataifa, naamini sasa tutaendelea kuwa salama kwa msimu mwingine ujao baada ya kuongeza watu wengine bora.”

SOMA NA HII  LUNYAMILA: KWA HILI LA NAMUNGO, TFF WANASTAHILI PONGEZI