Habari za michezo

WAKATI YANGA WAKIIALIKA VIPERS YA UGANDA …SINGIDA BIG STARS WAIALIKA TIMU HII KUBWA AFRIKA KWENYE SIKU YAO…

admin August 2, 2022 8:57 am


Wakati vigogo Yanga na Simba wakiwa bize kuelekea matamasha yao ya ‘Wiki ya Mwananchi’ na ‘Simba Day’, klabu ya Singida Big Stars nayo imetangaza kuja na tamasha lake ililolipa jina la ‘Singida Big Day’.

Tamasha hilo litafanyika Alhamisi Agosti 4 mwaka huu saa 5 asubuhi katika uwanja wa Liti mkoani Singida ikiwa ni siku mbili kabla ya Wiki ya Mwananchi (Agosti 6) na siku nne kabla ya Simba Day Agosti 8.

Klabu hiyo imetangaza uwepo wa tamasha hilo leo Agosti Mosi kupitia kurasa za mitandao yake ya kijamii na kueleza kuwa itakuwa siku malaum kwa timu hiyo.

Katika tamasha hilo, Singida Big Stars ambayo inajiandaa kukipiga Ligi Kuu msimu huu itacheza na Zanaco FC ya nchini Zambia katika uwanja wa Liti mjini Singida.

“Wapenzi na mashabiki wetu tunawatangazia rasmi kuhusu siku hii kubwa na maalum kwa timu yetu,”

“Karibuni mshuhudie kikosi kamili cha Singida Big Stars, benchi la ufundu bora zaidi, jezi zetu mpya za msimu ujao, mechi ya kirafiki dhidi ya Zanaco na mengine kibao,” imesema taarifa hiyo.

Singida Big Stars ambayo imeshanasa baadhi ya mastaa akiwemo Said Ndemla, Abdulmajid Mangalo, Metacha Mnata na Paul Godfrey ‘Boxer’ inaendelea kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu utakaoanza Agoati 17 ikiwa imeweka kambi yake jijini Arusha.

PATRICK AUSSEMS AKIMBIA TIMU KENYA….AISHIA KUWAPA MATUMAINI KWA ‘VIDEO CALL’…TIMU YA RWANDA YATAJWA KUHUSIKA… BAADA YA KUILAMBISHA YANGA MKATABA MNONO…SportPesa WAHAMISHIA MABILIONI YAO KWA SINGIDA BIG STARS….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply