Habari za michezo

KABLA KIZA HAKIJAWA KIKALI LEO…SIMBA KUSHUSHA KIFAA KINGINE CHA KAZI …NI STRAIKA LA MAGOLI HASWA…

admin August 5, 2022 2:44 pm


Kama ulikuwa unadhani wamemaliza jua unajiongopea, Wekundu wa Msimbazi Simba SC, leo Agosti 5, 2022 wanashusha jembe jipya la kazi katika safu ya ushambuliaji.

Hayo yamezungumzwa mapema hii leo na Msemaji wao, Ahmed Ally alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha radio cha Wasafi alipokuwa akizungumzia tamasha lao la Simba Day ambalo linatarajia kuchukua nafasi Agosti 8, 2022.

“Tunatarajia kutangaza mchezaji mwingine mpya hii leo ambaye atakuwa ni mshambuliaji,” alisema Ahmed.

Msemaji huyo alisema, baada ya kuachana na wachezaji watatu jana, Kagere, Wawa na Lwanga, wanazo nafasi mbili za kujaza idadi ya wachezaji wa kigeni ambapo moja wapo ndio hiyo wanayokwenda kuijaza.

Amesema, baada ya hapo wataangalia tena kama wanaweza kuongeza mchezaji mwingine wa kigeni au la.

Aidha, msemaji huyo alimzungumzia kiungo wao Kanuti ambaye hakuonekana na kikosi nchini Misri ambapo alisema alikuwa anashughulikia masuala yake ya Paspoti na sasa tayari yupo nchini na leo anatarajia kujiunga na wenzake kuendelea na mazoezi kwa ajili ya msimu ujao.

PAMOJA NA KUWA NA USAJILI MZURI…MASTAA WAPYA AZAM WAHAHA NA LUGHA…WENGI HAWAJUI KIINGEREZA… KUELEKEA MECHI YA NGAO YA JAMII…SIMBA WAANDAA SILAHA ZA SIRI KUIMALIZA YANGA…UKWELI WOTE HUU HAPA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply