TFF imewafungulia mashtaka ya kimaadili Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said & Haji Manara.
Manara anashtakiwa kwa kutoheshimu adhabu aliyopewa ya kutojihusisha na soka ndani na nje ya nchi kwa miaka miwili.
Hersi anashtakiwa kwa kushindwa kuhakikisha Yanga inaheshimu uamuzi huo.
โManara alifungiwa kujihusisha na shughuli yoyote ya mpira wa miguu lakini ameshindwa kutekeleza adhabu hiyo, naye Hersi amekwenda kinyume na katiba ya TFF na Yanga,โ imesema sehemu ya Taarifa hiyo.