Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezho, Mohamed Mchengerwa juzi tarehe 9, 2022 amemuagiza Katibu Mkuu wizara hiyo, Dk. Hassan Abbasi kumpangia majukumu mengine Meneja wa Uwanja wa Benjamini Mkapa, Godon Nsajigwa kwa kushindwa kusimamia matumizi ya uwanja huo.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku moja imepita baada ya Klabu ya Simba kuadhimisha sherehe za kilele ya Siku ya Simba ‘Simba Day’ na kuibu mjadala kuhusu baadhi ya burudani zilizotolewa na wasanii waliolikwa na klabu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, John Mapepele imesema Meneja huyo anapangiwa majukumu mengine kwa kushindwa kusimamia matumizi endelevu ya Uwanja wa Benjamini Mkapa.
Dk. Abbasi akieleza utekelezaji wa agizo hilo, amesema tayari taratibu zimekwishaanza za kupangiwa majukumu mengine nna nnafasiuo hiyo inatarajiwa kusazwa mara moja.
Itakumbukwa kuwa katika tamasha hilo la Simba Day lililofanyika jana Jumatatu tarehe 8 Agosti, 2022, msaani wa Bongofleva, -Khalid Ramadhani Tunda maarufu kama Tunda Man aliingia katika uwanja wa Benjamini Mkapa akiwa amebebwa katika jeneza pamoja na msalaba uliokuwa na maneno ya dhihaka kwa watani wao wa jadi Yanga yaliyosomeka “Kifo cha Utopolo.”
Staili hiyo ya Tundaman kuingia katika tamasha hilo, imebua mjadala na kuwaibua baadhi ya viongozi wa dini akiwamo Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Methodius Kilaini ambaye mapema leo amelaani kitendo cha klabu hiyo ya Simba kumruhusu msanii huyo kutumbuiza kwa kutumia msalaba na kufanya dhihaka.
Kitendo hicho Askofu Kilaini amesema ni “dharau na kufuru kubwa kwa waamini wakristu na wote wanaoamini walikombolewa katika msalaba huo.”