Habari za michezo

WAKATI BARBARA AKIWAKILISHA SIMBA KWENYE MKUTANO WA CAF…YANGA WAIBUKA NA HOJA HIZI BAADA YA KUTOPEWA MWALIKO….

admin August 11, 2022 3:25 pm


Uongozi wa Yanga umetoa kauli juu ya kutoalikwa katika Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), bado hawajajua sababu za kutopewa mualiko.

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Yanga wakili Simon Patrick akizungumza na kituo cha radio cha E-fm amesema wamelazimika kufuatilia mkutano huo kupitia mitandao baada ya kutopata mualiko.

Simon amesema Yanga ambao ni mabingwa wa nchi walitamani kuwepo katika mkutano huo unaonendelea jijini Arusha na kuhudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

“Bahati mbaya hatujajua kipi kimetokea na sisi (Yanga) kukosa mualiko, tuliamua kutumia fursa ya teknolojia tuweze kufuatilia mkutano huu,”amesema Simon.

“Ni jambo jema tunafurahi limerfanyika hapa Tanzania, kwa manufaa mapana ya nchi yetu wamepata kutangaza utalii, wamepata kujionea mazuri ya Tanzania.”

Aidha Simon ameongeza ingawa mkutano huo ni wa CAF lakini wanafahamu kwamba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ndio walipaswa kutambua nafasi ya Yanga kushiriki mkutano huo kwa kuwapa klabu yao mualiko.

KISA SIMBA NA YANGA ..SENZO KWA MARA YA KWANZA AIBUKA NA MSIMAMO HUU KUHUSU SOKA LA TZ… KISA KUACHWA NA SIMBA …DILUNGA AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA A-Z KUHUSU MKATABA WAKE…’BWALYA’ ATIA NENO….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply