Home Habari za michezo BAADA YA BUMBULI KUONYESHWA MLANGO WA KUTOKEA YANGA….KATI YA HAWA WANNE MMOJA...

BAADA YA BUMBULI KUONYESHWA MLANGO WA KUTOKEA YANGA….KATI YA HAWA WANNE MMOJA WAO KUMRITHI…


Siku moja baada ya Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga, Wakili Simon Patrick kukiri kuwa wameachana na aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Yanga, Hassan Bumbuli tayari tetesi zimezagaa kuhusu mrithi wa Nafasi hiyo..

Wakili Simon akihojiwa na kituo cha Uhai FM alikiri kuwa wameachana na Bumbuli baada ya Mkataba wake kumalizika na hivyo nafasi hiyo kwa sasa ipo wazi kwa yeyote mwenye vigezo anaruhusiwa kutuma maombi.

Sasa tayari kundi la wanahabari vijana wanatajwa kutuma maombi kutaka nafasi hiyo ambao ni Ali Kamwe, Juma Ayo (amekiri kutuma maombi), Ahmed Abdallah na mwanadada Prisca Kishamba.

Katika Majina hayo ambayo yameshatuma maombi mpaka wakati huu jina la Mwandishi wa habari za michezo kutoka kituo cha Azam Media Ali Kamwe linapewa kipaumbele kuchukua nafasi hiyo.

SOMA NA HII  ACHANA NA HABARI ZA UTAMBULISHO WA OUATTARA....HAYA HAPA YA UMUHIMU UNAFAA KUYAJUA KUHUSU USAJILI WAKE...