Geita Gold FC

KUMBE ILIBAKI HIVII TUUH MPOLE ASAINI MSIMBAZI….MWENYEWE AFUNGUKA DILI LILIVYOBUMA WAKAHAMIA KWA ‘MZUNGU’….

admin August 18, 2022 3:08 pm


Kinara wa upachikaji wa mabao msimu uliopita kwenye Ligi Kuu Bara, Mshambuliaji wa Geita Gold George Mpole amefunguka sababu za kushindwa kusaini Simba ni suala la maslahi tu.

Mpole ambaye tayari ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia Geita Gold amesema ni kweli alipokea ofa kutoka Simba lakini Geita walikidhi maslahi yake ndio maana hakuona umuhimu wa kuondoka klabuni hapo.

“Nilikuwa na ofa nyingi kutoka timu za ndani na nje ya Tanzania ila nimeamua kubaki kwa sababu wameweza kunitimizia mahitaji yangu.” amesema Mpole na kuongeza;

“Kuhusu kuzungumzwa kwamba nimechelewa kusaini mkataba na Geita Gold sio kweli, ni timu ambayo nashirikiana nayo kwenye kila kitu na suala la ofa zangu za nje taarifa hizo wanazo,” amesema.

Nyota huyo alikuwa sehemu ya kikosi cha Geita katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi Ligi Kuu Bara wakati timu yake ilipofungwa mabao 3-0 dhidi ya Simba jana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

MAPYA YAIBUKA SAKATA LA MANZOKI KUTUA MSIMBAZI…VIPERS NA WAKALA WAKE WAIVURUGA SIMBA… UKUTA WA YANGA KUTIKISIKA…..NABI ATOA MSIMAMO HUU KUHUSU KUWATUMIA JOB, MWNYETO AU BANGALA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply