Habar za Usajili Simba

MAPYA YAIBUKA SAKATA LA MANZOKI KUTUA MSIMBAZI…VIPERS NA WAKALA WAKE WAIVURUGA SIMBA…

admin August 18, 2022 2:49 pm


Wakati zikisaliwa takribani siku 13 kabla ya usajili wa dirisha kubwa kufungwa hapa nchini, uongozi wa Simba, umetangaza kuachana mazima na mshambuliaji wa Vipers FC ya Uganda, César Lobi Manzoki.

Hiyo ni katika kuelekea kufungwa kwa usajili Agosti 31, mwaka huu baada ya kufunguliwa Julai Mosi.

Awali Simba ilielezwa kumalizana na mshambuliaji huyo aliyetwaa Tuzo ya Ufungaji na Mchezaji Bora katika Ligi Kuu ya Uganda msimu uliopita kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi chao.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema baada ya kumtambulisha Mserbia, Dejan Georgijevic, hakuna mchezaji mwingine watakayemsajili kipindi hiki.

Aliongeza kuwa, kutokana na utata uliopo katika ukomo wa mkataba wa Manzoki na timu yake ambapo mwenyewe anasema unaisha Oktoba mwaka huu, huku Vipers ikisema utaisha 2024, ndiyo sababu ya kuachana naye.

“Kama uongozi tumechukua uamuzi wa kuachana na Manzoki, labda hadi katika dirisha dogo au msimu mwingine, hivyo Dejan ndiye amefunga usajili wetu.

“Manzoki mkataba wake haupo wazi kwa pande zote mbili, yeye mwenyewe anasema ana mkataba wa miezi miwili, lakini timu yake inasema ana mkataba hadi 2024.

“Hiyo imesababisha mazungumzo kuwa magumu, hivyo tumesitisha mipango hiyo ya kumsajili Manzoki kwa hivi sasa, labda yatokee mabadiliko mengine kabla ya usajili kufungwa,” alisema Ally.

KISA SARE MBILI  MFULULIZO….KLOPP AINGIA KWENYE KASUMBA ZA KURONGWA…ADAI WACHEZAJI WAKE WAMECHEZEWA… KUMBE ILIBAKI HIVII TUUH MPOLE ASAINI MSIMBAZI….MWENYEWE AFUNGUKA DILI LILIVYOBUMA WAKAHAMIA KWA ‘MZUNGU’….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

One response to “MAPYA YAIBUKA SAKATA LA MANZOKI KUTUA MSIMBAZI…VIPERS NA WAKALA WAKE WAIVURUGA SIMBA…”

  1. Cheapest Proxies says:

    What’s Going down i’m new to this, I stumbled upon this I’ve found It absolutely helpful and it has helped me out loads. I’m hoping to contribute & help different users like its helped me. Great job.

Leave a Reply