Home Habari za michezo MAKAMBO NA MORRISON WAPEWA WAJIBU MPYA YANGA…NI BAADA YA KUSHINDWA KUPATA NAMBA...

MAKAMBO NA MORRISON WAPEWA WAJIBU MPYA YANGA…NI BAADA YA KUSHINDWA KUPATA NAMBA KIKOSI CHA KWANZA…


Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi, amesema kuwa wachezaji wake, Mghana Bernard Morrison na Mkongomani, Heritier Makambo, wana kazi maalum za kimbinu na kiufundi katika kikosi chake.

Kauli hiyo aliitoa mara baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kumalizika dhidi ya Polisi Tanzania juzi Jumanne kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha. Yanga ilishinda 2-1.

Nabi alisema kuwa wachezaji hao anawatumia kama ‘Super Sub’ ambao kazi yao ni kwenda kuwazuia mabeki na viungo wakabaji wa timu pinzani kupanda.

Nabi alisema kuwa anawatumia wachezaji hao katika kipindi cha pili katika dakika za mwishoni kwa lengo la kuwachosha mabeki na viungo wakabaji wa wapinzani wao.

Aliongeza kuwa alianza kuwatumia katika mchezo wa Wiki ya Mwananchi waliocheza dhidi ya Vipers United ya Uganda, Kariakoo Dabi na huu wa Polisi ambao mabeki na viungo wa timu pinzani walikuwa nyuma wengi wakilinda goli lao.

“Mchezo wetu dhidi ya Polisi ulikuwa mgumu kutokana na mabeki na viungo wakabaji kukaa golini wengi wakilinda goli lao na hasa katika kipindi cha pili.

“Baada ya kuona mambo yanakuwa magumu nikachukua maamuzi ya kumuingiza Makambo ambaye kazi yake ilikuwa ni kuwazuia mabeki na viungo wa timu pinzani wasipande kuja kutushambulia na badala yake tuwashambulie wao.

‘Pia nikamuingiza Morrison ambaye yeye naye aliongeza kasi ya ushambuliaji kabla ya kupiga asisti yake iliyozaa bao la pili. Pia kuingia kwake kuliwafanya mabeki wa timu pinzani kujaa presha kubwa kutokana na kiwango chake alichonacho,” alisema Nabi.

SOMA NA HII  UMESIKIA HIYOO...TIMU ITAKAYOMTAKA 'JINI' HAALAND IWE NA TSH TRILIONI 2 ....