Home Habari za michezo MECHI YA KUFUZU CHAN DHIDI YA UGANDA…SIMBA NA YANGA ZASHINDANA KUTOA MAKIPA...

MECHI YA KUFUZU CHAN DHIDI YA UGANDA…SIMBA NA YANGA ZASHINDANA KUTOA MAKIPA NA MABEKI TAIFA STARS…


Kipa namba mbili wa Simba, Beno Kakolanya amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stas’ kitakachoingia kambini Agosti 21, 2022 kwa michezo miwili ya Kufuzu CHAN dhidi ya Uganda.

Kocha Mkuu Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza wachezaji 25 wa timu hiyo watakaoingia kambini kujiandaa na mechi ya kufuzu Fainali za mataifa ya Afrika (CHAN) huku akiwajumuisha wanne wapya.

Nyota wawili wa Azam, beki Nathanael Chilambo na kiungo Sospeter Bajana, wawili wa Simba kipa Beno Kakolanya na mshambuliaji Habib Kyombo ndio wachezaji wapya waliojumuishwa kwenye kikosi hicho huku wengine 22 wakiwa wale waliokuwepo kwenye kikosi cha mara ya mwisho.

“Wachezaji tuliowachukua tumezingatia viwango vyao vya hivi karibuni na nmewafuatilia wote na sasa tumechagua 25 tu na ndani yake kuna wapya wachache tu ukilinganisha na tuliokuwa nao kwenye mechi dhidi ya Somalia,” amesema Kim.

Mastaa walioitwa kwenye timu hiyo ni makipa Aishi Manula na Kakolanya kutoka Simba sambamba na Aboutwalib Msheri wa Yanga.

Mabeki ni Kibwana Shomari (Yanga), Shonari kapombe (Simba) ,Chilambo (Azam) Dickson Job (Yanga), Bakari Mwamnyeto (Yanga), Kennedy Juma na Mohamed Hussein (Simba) na Paschal Msindo wa Azam.

Viungo ni Jonas Mkude, Mzamiru Yassin na Kibu Denis kutoka Simba, Kelvin Nashon wa Geita Gold, Sospeter Bajana, Abdul Seleman Sopu wa Azam pamoja na Salum Abubakari, Farid Mussa na Feisal Salum wa Yanga.

Washambuliaji ni Kyombo wa Simba, Daniel Lyanga na George Mpole wa Geita, Anwary wa Kagera sambamba na Reliants Lusajo kutoka Namungo.

Taifa Stars itaanza mazoezi rasmi Jumatatu ya Agosti 22 na itacheza mechi ya kwanza ntumbani Agosti 28 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na mechi ya marudiano itapigwa Septemba 3, 2022 nchini Uganda.

SOMA NA HII  LANGONI KWA RIVERS KUNAWAKA MOTO...YANGA KUWENI MAKINI MTAUMIA