Home Habari za michezo YANGA WAZIDI KULISHIKA SOKA LA BONGO KIVYAO VYAO….USHINDI DHIDI YA COASTA JANA...

YANGA WAZIDI KULISHIKA SOKA LA BONGO KIVYAO VYAO….USHINDI DHIDI YA COASTA JANA WAIPA REKODI HII YA KUDUMU….


Klabu ya Yanga imeandika rekodi mpya Ligi Kuu Bara ya kucheza mechi 39 bila kupoteza baada ya kuifunga Coastal Union mabao 2-0 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Timu hiyo msimu uliopita 2021/22 ilichukua Ubingwa wa Ligi Kuu NBC bila kupoteza mechi hata moja ilizocheza za ligi na na kuanza msimu kwa ushindi wa mechi zake mbili na kufanya kufikia idadi hiyo.

Awali Yanga ilikuwa inashikilia rekodi hiyo sawa na Matajiri wa Chamazi Azam FC ya kucheza mechi 38 bila kupoteza ambapo Azam ilifanya hivyo kati ya Feb 23, 2013 hadi Oktoba 25, 2014 huku Yanga ikiweka rekodi hiyo kati ya Mei 15, 2021 hadi  Agosti 16, 2022 kabla ya jana kuandika rekodi mpya.

Katika mchezo dhidi ya Coastal ilichukua Dakika 4 tu za mchezo kabla mchezaji wa Yanga Bernard Morrison kufungua dimba kwa bao la kwanza baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Jesus Moloko.

Katika mchezo huo, Dakika ya 55 alitoka Makambo na kuingia mshambuliaji tegemezi wa Yanga Fiston Mayele aliyechangamsha mchezo na kupelekea dakika ya 68 kupata bao la pili kwa kupiga kichwa mpira uliorudishwa kwenye eneo la hatari na beki Shaban Djuma.

Katika mchezo huo kadi za njano zilitawala ambapo dakika ya 12 wachezaji Mtenje Albano alizawadiwa kadi ya njano baada ya kumkanyaga Yanick Bangala aliyejibu mapigo kwa kumsukuma mchezaji huyo naye akaambulia kadi hiyo hiyo.

Dakika ya 32 mchezeshaji wa Yanga Morrison nae alioonyeshwa kadi ya njano kwa kosa la kutaka kumhadaa mwamuzi kwa kujiangusha eneo la hatari.

Dakika ya 53 Aucho alipewa kadi ya njano na kuifanya Yanga kuvuna kadi ya tatu ya njano baada ya kumchezea madhambi Mtenje Albano wa Coast na Dakika ya 62 kocha msaidizi wa Yanga Cedric Kaze akipaonyeshwa kadi nyingine baada ya kusimama na kuonyesha hasira kwa kupiga kopo la maji teke.

SOMA NA HII  KUHUSU BANGO LA 5G LA YANGA....SIMBA WAAMUA KUCHUKUA HATUA HIZI MAPEMAA...