Kocha wa klabu ya Chelsea, Thomas Tuchel hana haraka ya kurudi tena sokoni ili kuimarisha kikosi chake kwa kuingiza maingizo mapya ya wachezaji ili kuimarisha kikosi hicho kilichopoteza kwenye mchezo wa jana dhidi ya Leeds kwa goli 3-0.
Awali Tuchel alinukuliwa kuwa alikuwa anaangalia uwezekeno wa kupata wachezaji wa daraja la juu kwenye nafasi ya mlinzi wa kati na mshambuliaji kwenye kikosi chake lakini hawezi kurupuku kununua kwa kupaniki.
Mpaka sasa klabu ya chelsea imesajili wachezaji wachache kuliko wachezaji waliondoka ambapo wamefanikiwa kumsajili Kalidou Koulibaly kutoka Napoli huku Antonio Rudiger na Andreas Christensen wakiondoka bure kwenye dirisha hili.
“Dirisha la usajili bado liko wazi na litakuwepo, tunachohitaji ni kungalia nini tunacho na nini tunaweza fanya,” Tuchel alimwambia mwandishi baada ya mchezo wao dhidi ya Leeds.