Habari za michezo

KISA SIMBA KUITWA ‘MAKOLO’…OSCAR OSCAR AFURA KWA MANENO NA KUMSHUKIA MANARA JUMLA JUMLA…

admin August 25, 2022 6:00 pm


Mchambuzi nguli wa masuala ya Soka nchini, Oscar Oscar ‘Mzee wa kaliuwa’ ameonyesha kutofurahishwa na kitendo cha aliyewahi kuwa Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara kuwapa jina la utani la ‘Makolo’ klabu yake hiyo ya zamani.

Akizungumza katika kipindi cha Jioni ya Leo kinachoruka kupitia E-Radio kuhusu Manara kutimiza mwaka mmoja baada ya kuhamia Yanga, Oscar amesema licha ya kuwepo majina mengi ya utani, lakini ‘Makolo’ ni jina baya ambalo yeye hapendi hata kulisikia.

“Kitu ambacho sikukipenda kwenye move ya Haji Manara kutoka Simba kwenda Yanga ni kufika na kuwaita Simba ‘Makolo’. Nadhani ni moja ya majina ninayoyachukia sana, na Haji amekuwa muasisi wake.

“Hata kama ni utani lakini kama kuna kitu nilikichukia kwenye move ya Haji, ni kuwaita Simba Makolo. Likolo hata hujui ni li kitu gani ambalo linazungumzwa, naliona ni li kitu tu ambalo halina mpango wowote, nadhani hiyo haikuwa nzuri.

“Haji lazima awe na heshima…. Lakini katika maneno yote na utani wote wa Simba na Yanga ambao wametaniana, hii Kolo imekaa vibaya, hii inasumbua sana haijakaa vizuri, anatakiwa awe na heshima,” amesema Osacr.

ILE SINEMA YA USAJILI WA KIUNGO MPYA MNIGERIA SIMBA IKO NAMNA HII AISEE…MWENYEWE KAFUNGUKA A-Z WANAOKWAMISHA DILI.. DILI LA MANZOKI KWA SIMBA…TAARIFA MPYA HII HAPA…NIPASHE WASANUA KILA KITU YALIYOMO NYUMA YA PAZIA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

One response to “KISA SIMBA KUITWA ‘MAKOLO’…OSCAR OSCAR AFURA KWA MANENO NA KUMSHUKIA MANARA JUMLA JUMLA…”

  1. Hyera says:

    Updates are all what we want here, thank you so much

Leave a Reply