Home Habari za michezo BAADA YA KUACHWA NA AZAM FC…MUDATHIR YAHYA ACHUKUA MAAMUZI MAGUMU…AJIWEKA KANDO NA...

BAADA YA KUACHWA NA AZAM FC…MUDATHIR YAHYA ACHUKUA MAAMUZI MAGUMU…AJIWEKA KANDO NA SOKA JUMLA JUMLA…


Kiungo wa zamani wa Azam FC, Mudathir Yahya amedai anapumzisha mwili wake kipindi hiki ligi ikiwa inaendelea kwa kuwa karibu na familia yake.

Mudathir amefunguka hayo baada ya kumaliza mkataba na Azam FC ambaye amedumu kwa misimu 12 ndani ya timu hiyo na kutwaa taji moja la ligi.

Akizungumza Mudathir alisema: “Nina uwezo wa kucheza msimu huu kwani dirisha bado halijafungwa na nimepata ofa kutoka timu mbalimbali ambazo nimezifahamisha kuwa nahitaji kupumzika kwa muda hadi dirisha dogo litakapofunguliwa.

“Naifahamu vizuri ligi ya Tanzania kwani nimecheza muda mrefu zaidi kuachwa na Azam FC haina maana kwamba kiwango changu kimeshuka nipo vizuri na naweza kucheza timu yopyote ambayo inaweza kunisajili.”

Mudathir alisema pamoja na kuamua kupumzika atakuwa anafanya mazoezi binafsi ili kujiweka fiti ili atakapoamua kurudi uwanjani asiwe na kazi kubwa ya kufanya hasa kupunguza mwili.

“Unajua mtu akiamua kupumzika anaweza akawa anakula na kulala muda mwingi, ni rahisi kuongeza mwili na kilo kuongezeka hivyo kwa mchezaji inaweza kuwa shida. Sitaki kukutana na changamoto hiyo nitafanya mazoezi kama kawaida,” alisema nyota huyo aliyedumu muda mrefu Azam FC.

SOMA NA HII  SIMBA NA YANGA WALIVYOICHANGAMSHA CAF KIBABE...UMAARUFU WAPANDA KWA KASI...