Home Azam FC BAADA YA MIEZI KADHAA YA KUAMINIANA…AZAM FC NA KOCHA WAO MSOMALI WAFIKISHANA...

BAADA YA MIEZI KADHAA YA KUAMINIANA…AZAM FC NA KOCHA WAO MSOMALI WAFIKISHANA HATUA HII….


Tumefikia makubaliano ya pande mbili na kocha wetu, Abdihamid Moallin, na msaidizi wake, Omary Nasser, kuachia ngazi kama kocha mkuu na msaidizi mtawalia.

Hata hivyo, makocha hao wataendelea kubaki kama sehemu ya idara ya ufundi klabuni kwetu katika nafasi nyingine ambazo tutazitangaza hapo baadaye.

Kwa sasa timu itakuwa chini ya Daniel Cadena, ambaye ni kocha wa makipa, hadi tutakapotangaza kocha mpya.

Cadena ni kocha mwenye leseni ya juu kabisa ya ukocha, UEFA Pro License.

SOMA NA HII  ACHANA NA STORI ZAKUOKOTEZA HUKO....KOCHA WA SIMBA QUEENS KAENDA MALAWI KWA KAZI HII MAALUMU TU....