Home Habari za michezo CAF WAIPA TANZANIA ‘KAMSELELEKO’ KUWANIA KUFUZU AFCON MWAKANI…RATIBA YOTE KAMILI IKO...

CAF WAIPA TANZANIA ‘KAMSELELEKO’ KUWANIA KUFUZU AFCON MWAKANI…RATIBA YOTE KAMILI IKO HAPA…


Tanzania imepangwa kuanza na Sudan Kusini katika mashindano ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 23 (AFCON U23) zitakazofanyika Morocco mwakani.

Fainali hizo za AFCON U23 mwakani zitashirikisha jumla ya timu nane (8) ambazo zitasaka nafasi tatu za kuiwakilisha Afrika katika michezo ya Olimpiki 2024 itakayofanyika Paris, Ufaransa.

Tukio la uchezeshaji droo wa mashindano hayo ya kufuzu, limefanyika juzi katika makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) huko Cairo Misri ambapo kwa mujibu wa droo hiyo, Tanzania U23 itaanzia nyumbani na kisha kumalizia ugenini ambapo mechi zote zitachezwa mwezi ujao.

Ikiwa Tanzania U23 itafanikiwa kusonga mbele dhidi ya Sudan Kusini, katika raundi ya pili  itakutana na Nigeria ambayo imefuzu moja kwa moja katika hatua hiyo bila kucheza mchezo wowote kutokana na nafasi nzuri waliyopo katika viwango vya ubora wa soka vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA).

Na kama itasonge mbele tena dhidi ya Nigeria, katika raundi ya tatu na ya mwisho itaumana na mshindi baina ya timu za Uganda na Guinea na mshindi wa hapo atasonga mbele kushiriki Afcon U23.

Tanzania U23 imekuwa na bahati mbaya ya kushindwa kufuzu fainali za AFCON U23 ambapo mara zote ilizoshiriki iliishia katika mechi za kuwania kufuzu

Katika mashindano ya kufuzu fainali zilizopita za mwaka 2019 zilizofanyika Misri, Tanzania U23 ilitolewa na Burundi katika raundi ya kwanza na ilipowania kufuzu fainali za mwaka 2011 zilizofanyika Morocco, ilikomea katika raundi ya mwisho ambapo ilitolewa na Nigeria.

SOMA NA HII  BAADA YA KUSOTEA BENCHI SANA...YANGA WAAMUA KUACHANA NA 'NINJA' KWA STAILI HII MPYA...AKIZINGUA NDIO BASI TENA...